24
Sun, Mar
2 New Articles

Top Stories

Grid List

Destroyed strategy missing afford

Press Release

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea taarifa zinazohusu askari polisi kuwapiga na kudhalilisha watu wenye ulemavu katika tukio lililotokea asubuhi ya Juni 16, 2017, Mtaa wa Sokoine jijini Dar es Salaam.Pakua Habari kamili.

 

 

 

 

 

Crime affected citizen thoughts

Press Release

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu uvamizi wa kituo cha Luninga na Radio cha Clouds Media Group, uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, usiku wa tarehe 17, Machi mwaka huu, akiwa na askari wenye silaha.

Canada reader forget shaking favorite

Press Release

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Kampuni ya RAHCO cha kubomoa nyumba zaidi ya 200 zilizojengwa pembezoni mwa reli maeneo ya Buguruni siku ya Jumamosi tarehe 11 Machi 2017, baada ya wakazi kutangaziwa ubomoaji huo siku moja kabla, wakati RAHCO wakiwa na taarifa ya wito wa
Tume kuhusu uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuhusu uhalali wa makazi yao kuwa nje ya mita 15 au mita 30 kama Sheria ya Reli, Namba 4 ya mwaka 2002 inavyoelekeza kwa maeneo ya mjini na vijijini.

Zoezi hilo Iilianza tarehe 11/03/2017 saa nne asubuhi katika mtaa wa Madenge Kata ya Buguruni, na Iimeendelea tarehe 12/03/2017 katika mitaa ya Faru, Mtakuja na Mtambani katika Kata ya Mnyamani.
Mnamo tarehe 22 Februari 2017 Kamati iIiyoundwa na wanachi wa Mnyamani walifika Tume na kusajili Ialamiko kwamba nyumba zao ziliwekwa alama ya X kuashiria kuvunjwa
bila wao kupewa taarifa, na walipouliza waliambiwa kuwa zitavunjwa tarehe 16 Machi 2017.
Tume iIifanya mawasiliano na Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani, Faru na Diwani wa Mnyamani kutaka kujua usahihi wa malalamiko ya wananchi, na taarifa za RAHCO
kutaka kuvunja nyumba, Iakini viongozi wa mtaa waliiambia Tume kwamba hawakuwa na taarifa toka RAHCO kama watabomoa nyumba hizo. Tume iIiwasiIiana na RAHCO ambao walisema kwamba eneo hilo ni Ia mradi wa reli ya “Standard gauge” ambao ni mradi muhimu kitaifa na wakadai kuwa ramani ya mipango miji inaonyesha kuwa eneo Ia
Mnyamani Iiko ndani ya mita 30 tofauti na wanachi walivyodai.
Baada ya mawasiliano hayo ya awali Tume iIiiandikia pande zote mbili barua mnamo tarehe 7 Machi 2017 na kuzitaka zilete vielelezo vyao Tume ifikapo tarehe 13 Machi 2017
na ikatoa wito kwa pande zote mbili iIi zifike mbele ya Tume na kusikilizwa tarehe 14 Machi 2017. Baada ya kupata barua ya Tume, RAHCO waliijibu Tume kwamba
wasingeweza kuleta vielelezo eti kwa sababu mwanasheria wao alikuwa safari.
Lakini walikiri kuwa:

“Zoezi hilo ambalo lilifanyika kwa mara nyingine tarehe 17 Februari 2017 lilishirikisha wawakilishi mbalimbali kutoka Manispaa, taarifa hiyo iIiwasiIishwa ofisi ya Mkoa na Wilaya
husika. Aidha wawakilishi kutoka Serikali za Mitaa hawakuwepo katika zoezi hilo. Haijulikani ni kwa sababu gani ushiriki wao haukuwepo”. Barua hiyo iIiyopokeIewa Tume
tarehe 9 Machi 2017 ilieleza.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inawataka Watanzania na mamlaka kwa ujumla kutambua kwamba, Tume ni taasisi iIiyoundwa ndani ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kusimamia haki za binadamu na misingi ya utawala bora. Tume imepewa mamlaka na Katiba kufanya uchunguzi wa malalamiko ya
wananchi kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora.

Tume inatambua, kama mwananchi mwingine yeyote, kuhusu umuhimu wa maendeleo ya nchi, umuhimu wa miundombinu ya kisasa ikiwemo reli ya mwendo kasi. Lakini pia
inaamini kuwa iIi utawala wa sheria udumishwe nchini, lazima kiIa mtu na taasisi zote za umma na binafsi ziheshimu utawala wa sheria. Msingi mmoja mkuu wa Utawala Bora ni utii wa sheria.

Kwa hiyo, maamuzi na hatua zozote za utekelezaji wa maendeleo ya wananchi yanapochukuliwa lazima yazingatie haki za wananchi. Msingi mkuu wa maendeleo na mlengwa mkuu wa maendeleo ni watu.

Tume imesikitishwa na kitenda cha RAHCO kudharau wito wa Tume na kujichukulia sheria mkononi na kuvunja nyumba za wananchi bila kuwapa haki ya kusikilizwa kama
ambavyo Tume iIikwishapanga. Haki hupatikana pande mbili zikisikilizwa, siyo kwa kutumia ubabe wala kwa tafsiri ya sheria ya upande mmoja.

Kwa uvunjaji huu uliofanywa na RAHCO, hususani katika eneo Ia Mnyamani, wakati wakijua kuna kikao cha uchunguzi, na kitendo cha kufanya uvunjaji kabla ya siku
wananchi waliyoambiwa, ni uvunjaji wa haki ya msingi ya mtu kupewa muda wa kutosha (notisi), na ni kujichukulia sheria mkononi.

Kifungu na 14(2) cha Sheria ya Tume namba 7 ya 2001 Sura 391 kinazitaka mamlaka zinazo Ialamikiwa kushirikiana na Tume kupata ukweli na haki iIipo, na Tume ina wajibu
wa kutoa mapendekezo kwa mujibu wa Katiba, sheria na kanuni husika baada ya kusikiliza pande zote. Tusipofanya haya hatutajenga utamaduni wa kuheshimu, utawala
wa sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala bora

Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inatambua haki ya kiIa mtu kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria. Pia Ibara ya 18 (b) inatambua haki ya kila mtu kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu ya jamii. Ibara ya 24 inatambua haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria na kunyanganywa mali, ikibidi, kwa mujibu wa sheria. Tanzania ikiwa nchi ambayo imeridhia mikataba ya kimataifa na ya kikanda ya haki za binadamu, inawajibika kulinda haki za wananchi kwa kuhakikisha kwamba hawatendewi vitendo vya kuwadhaiilisha.

Uvunjaji wa makazi na uharibifu wa mali za watu uliofanywa na RAHCO, jambo ambalo Iimewatia wananchi wengi ufukara ni kuhatarisha haki ya kuishi ambayo ni haki ya msingi inayotambulika kikatiba, na hata katika sheria za kimataifa. Vitendo hivi (forced eviction) vinapingwa na maazimio na mikataba ya Umoja wa Mataifa ambayo Tanzania
imeyakubali.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inafanya na kusema haya kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Ibara 130 (1)(c) na (f) vinavyoipa
mamlaka kufanya uchunguzi juu ya mambo yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora; na kuchunguza mwenendo wa mtu yeyote
anayehusika au taasisi yoyote inapokiuka hayo katika utekelezaji wa kawaida wa madaraka ya kazi au majukumu yake.
Tume itaendelea kufanya uchunguzi wake kama ilivyopanga hapo tarehe 14 machi 2017.
Imetolewa na:

k.n.y.
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Machi 13, 2017

Hotuba ya Mheshimiwa Bahame Tom Nyanduga, Mwenyekiti wa Tume katika siku ya kupinga mateso na ukatili dhidi ya wazee duniani, tarehe 15 Juni 2017, yaliyofanyika katika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jengo la Haki, Dar es Salaam. Pakua hotuba kamili

Hotuba ya Mhe. Bahame Tom Nyanduga, Mwenyekiti wa Tume wakati wa hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari tanzania (EJAT) 2015, ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, aprili 29, 2016. Pakua hotuba kamili

Hotuba ya mwenyekiti wa Tume Mhe. Bahame T. Nyanduga, katika ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu mikakati ya kukomesha mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi , tarehe 18 Machi 2015 katika ofisi za Tume. Pakua hotuba kamili

Mkurugenzi wa Sheria kutoka taasisi ya Sheria Kiganjani, Jumanne Nabir (kulia) akimuonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Alexander S. Hassan (katikati) namna ya mfumo wa sheria kiganjani unavyofanya kazi. Kushoto anayeangalia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria kutoka Tume, Nabor Assey.

News

Ujumbe wa taasisi ya Sheria Kigangani  umeitembelea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(THBUB) machi, 12, 2019.

Akiongea katika kikao  kifupi baina ya taasisi hizo,  Mkuu wa msafara huo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria wa taasisi hiyo ya Sheria Kiganjani, Jumanne Nabir  alisema kuwa lengo la ziara yao ni kujieleza na kujitambulisha kwa tume na kuona uwezekano wa kuanzisha ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.

“Lengo la ujio wetu kwenu ni kujitambulisha  ili muijue  Sheria Kiganjani, namna inavyofanya kazi na faida zake kwa jamii na kuona uwezekano wa kushirikiana nanyi” alisema Nabir

Nabir aliendelea kueleza kuwa  sheria kiganjani ni mfumo unaomuwezesha mtu kupata huduma za kisheria kupitia simu yake ya mkononi.

“Mtu anaweza kupata huduma hii kupitia simu aina zote, simu za kawaida na smartpone, kwa sasa tupo katika utafiti na tangu tumeanza kazi mwaka jana mpaka sasa wamepatikana watumiaji elfu arobaini na tano (45,000) " aliongeza Nabir

Mkurugenzi huyo wa Sheria aliendelea kusema kuwa kupitia mfumo huo mwananchi anapata fursa ya kuunganishwa na mawakili kupitia simu yake popote nchini.

Kwa upande wa tume, Kaimu Katibu Mtendaji, Alexander S. Hassan aliipongeza taasisi hiyo kwa kuwa na ubunifu huo wa kuwasaidia  na kuwarahisishia watanzania kujua na kupata msaada wa sheria. 

Pia, aliuambia ujumbe huo kuwa tume inapata changamoto katika maeneo mawili ambayo ni namna ya kujitangaza na kutambulika kwa wananchi na pili ni namna ya kupata malalamiko yanayohusu uvunjwaji wa haki za binadamu nchini.

Kufuatia ujio wao, Hassan aliwaeleza kuwa tume inaona uwezekano wa kufanya kazi na Sheria Kiganjani upo, hivyo aliwataka wakamilishe taratibu za kuomba ushirikiano na tume ili kuwezesha kuanza kwa ushirikiano huo.

Ujumbe wa taasisi ya Sheria Kiganjani ulijumuisha watu wane (4) ambao ni Mkuu wa msafara, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria, Jumanne Nabir, Afisa Masoko, Brian Mallya, Afisa mifumo ya kompyuta, Mussa Kisena na Meneja Mradi, Chris Bwemo.

Sheria Kiganjani ni taasisi iliyoanzishwa na vijana wa kitanzania mwaka 2018 ambayo imetengeneza mfumo unaomuwezesha mwananchi wa kawaida kupata huduma za kisheria kupitia zimu yake ya mkononi, tovuti na mfumo wa  sms.

Mwisho.

Picha hapo juu ni Bw. Stanley Kalokola wakati akiwaelekeza Wasaidizi wa Kisheria namna ya kutuma malalamiko THBUB kwa kutumia njia ya ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) wakati mafunzo yaliyofanyika Kituo cha wasaidizi wa kisheria kilichopo Momba mkoani Songwe.

News

Wasaidizi wa sheria (paralegals) waliopo Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe  wameelimishwa namna ya kuwasilisha lalamiko Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  kupitia simu ya kiganjani.

Wasaidizi hao wa kisheria wapatao kumi na mbili (12) walipata elimu hiyo katika warsha iliyoandaliwa na Tume Februari, 21-22, 2019 katika ofisi za kituo cha wasaidizi wa sheria kilichopo Momba, Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Mkoani Songwe.

Akiongea katika warsha hiyo, Muwezeshaji, Afisa Uchunguzi wa Tume, Stanley Kalokola alisema kuwa Tume imeanzisha mfumo huu wa kuwasilisha lalamiko kupitia simu ya kiganjani ili kuwarahisishia wananchi na kuwapunguzia gharama na kuokoa muda.

Kalokola aliendelea kuwaeleza wasaidizi hao kuwa mfumo huo wa mawasiliano ni kwa njia ya meseji tu na haipaswi kupiga kwani haitapokelewa.

“Mwananchi mwenye lalamiko lake au taarifa kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu au ukiukwaji wa misingi ya utawala bora anaweza kutuma ujumbe wa simu ya kiganjani kwenda namba 0737 446 787,” alisema Kalokola

Kalokola alifafanua kuwa kupitia utaratibu huo, mara baada ya lalamiko au taarifa kufika tume, Afisa wa Tume atakayelipokea anaweza kupiga simu kwa mlalamikaji ili kupata maelezo zaidi kabla ya kuanza kushughulikia lalamiko hilo.

Aidha, Kalokola aliwaeleza wasaidizi hao wa sheria kuwa ili lalamiko liweze kufika kwa usahihi, mwananchi anatakiwa kuandika lalamiko lake kwa ufupi na kulituma kwa kuanza na neno ‘REPORT’ kwenda 0737 446 787.

Mbali na kuwasilisha lalamiko kwa tume kupitia simu ya kiganjani, mlalamikaji anaweza pia kuwasilisha lalamiko lake kwa kufika katika ofisi za Tume au kuandika barua ya lalamiko lake na kuituma kwa njia ya Posta.

MWISHO.

Kaimu Katika Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Hajjat Fatuma I. Muya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi kilichofanyika feb. 5, 2019, 

News

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), inategemea kuwa na ushirikiano wa kikazi baina yake na shirika la kimataifa lijulikanalo kwa jina la National Democratic Institute (NDI). 

Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB Hajat Bibi Fatuma I. Muya kwenye kikao kazi kilichohusisha baadhi ya watumishi wa Tume na Maafisa watatu (3) kutoka shirika la NDI. 

Akiongea kwenye kikao hicho Afisa wa NDI Bi. Juliana Brother alisema shirika la NDI llinalenga kushirikiana na Tume kwenye masuala ya Haki za Binadamu na utawala bora.

Pamoja na kueleza majukumu ya Tume Bibi. Fatuma pia aliwashukuru maafisa wa NDI kwa kuwa tayari kutanya kazi na Tume, hasa katika masuala ya haki za binadamu na utawala bora.

Kikao kazi hicho kilichofanyika tarehe  5 Februari, 2019 katika ofisi za Makao Makuu ya Tume Jijini Dar es salaam kilihusisha pia baadhi ya maafisa wa Tume kutoka Idara ya Sheria, Utawala Bora na  Haki za Binadamu.

Washiriki wengine ni Bi. Sarolly Quibaya na Bi. Mahiga Dodd  wote kutoka shirika la NDI.

 

 

TUNAPENDA KUWATANGAZIA WADAU NA WATEJA WOTE WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWAMBA OFISI ZETU ZILIZOPO JENGO LA TANCOT ZIMEHAMIA JENGO LA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA MTAA WA MKWEPU. HIVYO HUDUMA ZOTE ZITATOLEWA HUKO KUANZIA TAREHE 01 JANUARI, 2019

UTAWALA

Kamati ya Uteuzi ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, iliyoundwa na Ibara ya 129(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inautangazia umma kwamba, kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 7 cha Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura ya 391 Toleo la 2002 na Masharti ya Kanuni ya 6 na 7 za Kanuni na Uteuzi wa Makamishna za Mwaka 2001, Waombaji wa Kazi katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora waliooredheshwa katika Tangazo hili ndiyo yaliopitishwa na Kamati kwa madhumuni ya kusailiwa.

The Appointments Committee for Appointment of Commissioners, established under Article 129(4) of the Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 [as amended], hereby invites applications from suitably qualified Tanzanian citizens to apply for the posts of Chairperson, Vice Chairperson and Commissioners in the Commission for Human Rights and Good Governance.

Advertisement