03
Mon, Aug
3 New Articles

Jaji Mwaimu awataka watumishi tume kudumisha ushirikiano

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu an Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu akiongea na watumishi wa tume (hawapo pichani) katika hafla fupi iliyoandaliwa na Tume kuwakaribisha viongozi hao. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed Khamis. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume, Hajjat Fatuma Muya na Kamishna, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande.

News
Typography

Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amewasihi watumishi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kutobweteka na elimu ambayo tayari wanayo na badala yake wafanye jitihada za kujiendeleza pale inapobidi kufanya hivyo.

Mwenyekiti huyo mpya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora alitoa kauli hiyo katika hafla fupi ya kuwakaribisha viongozi wateule katika ofisi za makao makuu ya tume zilizopo jijini Dodoma Novemba 11, 2019.

 

Akizungumza na watumishi hao, Mwaimu aliwataka wafanye kazi kwa bidii na wapende kujiendeleza kwani elimu haina mwisho.

“Usiamini ulichonacho kinatosha, tupende kujiendeleza pale inapobidi, elimu haina mwisho hivyo tuweke jitihada na tuendelee kujifunza”alisema Mwaimu

Aidha, Mwaimu aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya utawala bora ikiwemo kuwahi kazini na kutumia taaluma zao ili kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

“Tujenge mahusiano mazuri kazini, tuwasiliane kwa madhumuni ya kuboresha utendaji kazi wa taasisi, ukiwa na jambo usikae nalo mwenyewe, tuwasiliane ili kutafuta ufumbuzi wa pamoja”aliongeza Mwaimu

Hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na ofisi ya tume ililenga kuwakaribisha Mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti na Makamishna wengine watano.

 

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.