03
Mon, Aug
3 New Articles

Jaji Mwaimu Mwenyekiti mpya THBUB

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu (katikati-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wateule wenzake. Kulia ni Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mohamed Khamis Hamad, Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji, Hajjat Fatuma Muya. Wengine waliosimama kutoka kushoto ni Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande, Mheshimiwa Thomas Masanja, Mheshimiwa Amina Talib Ali na Dkt. Fatma Rashid Khalfan.

News
Typography

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli amemteua Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti  wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).

Jaji Mwaimu aliteuliwa Oktoba, 2019 na kuapishwa rasmi Novemba 4, 2019 katika hafla  fupi ya kuapisha viongozi wateule iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Jaji Mwaimu aliapishwa pamoja na Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mohamed Khamis Hamad na Makamishna wengine watano (5).

 Makamishna hao watano ni  Mheshimiwa,  Dkt. Fatma Rashid Khalfan, Mheshimiwa Thomas Masanja,  Mheshimiwa Amina Talib Ali, Mheshimiwa Khatib Mwinyi Chande  na Mheshimiwa Nyanda Josiah Shuli.

Akizungumza na watumishi wa Tume katika kikao kifupi cha kuwakaribisha viongozi hao wateule kilichofanyika katika ofisi za THBUB zilizopo jijini Dar es Salaam, Jaji Mwaimu aliwataka watumishi  wote wa Tume  kuwa na ushirikiano  mzuri katika utendaji kazi wao wa kila siku.

“Inapendeza kuwa na watumishi   wenye bidii na umoja kazini ili kuleta ufanisi mzuri katika kazi”, alisema Jaji Mwaimu

Jaji Mwaimu anafanya idadi ya wenyeviti waliohudumu Tume kufikia wanne (4) tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa. Jaji Mwaimu anachukua nafasi hiyo ya Mwenyekiti iliyoachwa na mtangulizi wake Mheshimiwa Tom Nyanduga aliyemaliza kipindi chake.

 

Sign up via our free email subscription service to receive notifications when new information is available.