04
Tue, Aug
3 New Articles

Afisa wa THBUB afariki

Marehemu Getrude Alex pichani enzi za uhai wake

News
Typography

Getrude Alex (40), Afisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora amefariki dunia usiku wa Novemba 23, 2019 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Marehemu alikutwa na umauti baada ya kupata ajali ya kugongwa na pikipiki Novemba 21, 2019 katika eneo la ubungo jijini Dar es Salaam na kukimbizwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.

 

Marehemu aliajiriwa na tume Oktoba 18, 2010 kama Afisa Uchunguzi mwenye taaluma ya habari, na mpaka kifo kinamkuta alikuwa amehudumu katika taasisi hiyo kwa takribani miaka tisa (9).

Historia yake ya maisha inaonesha kuwa marehemu alikuwa mama wa watoto watatu wa kiume ambao ni Tupendane, Mbarikiwa na Baraka.

Kitaaluma marehemu alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (SJMC) mwenye Shahada ya Habari (2007).

Marehemu alizaliwa jijini Mwanza Julai 7, 1979. Alianza masomo shule ya msingi Kirumba (1989-1995), baadae alichaguliwa na kujiunga Mwanza Sekondari ambapo alimaliza elimu ya kidato cha nne (1996-1999).Kidato cha sita alimaliza katika shule ya Sekondari Tagwa (2000-2003).

Marehemu ataendelea kukumbukwa kwa wema wake, ucheshi, ushirikiano wake kwa watumishi hasa katika mambo ya kijamii na ukarimu.

Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.