20
Mon, Jan
6 New Articles

THBUB yatembelea AZAKI washirika

Afisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mbaraka Kambona (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya SIFO alipoitembelea taasisi hiyo Septemba 26, 2019. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa SIFO, Juma Issa Ngaona, wa pili kutoka kushoto ni Afisa Programu wa SIFO, Kissonga Mario na wa pili kutoka kulia ni Katibu wa SIFO, Hashim Mohamed.

News
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) hivi karibuni ilifanya ziara ya kutembelea Asasi za Kiraia ishirini (20) ambazo iliingia nazo mkataba wa ushirikiano zilizopo katika mikoa ya Tanzania bara na visiwani.

 

Katika ziara hiyo ambayo ilifanyika kuanzia Septemba 23-28, 2019 tume ililenga kuzitembelea asasi hizo ili kubadilishana mawazo na uzoefu wa utendaji kazi wa kila siku.

Taasisi ambazo zilitembelewa ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Taasisi ya Haki za Binadamu na Biashara (THRB), Taasisi ya Under the Same Sun (UTSS), Social Information and Facilitation Organization (SIFO).  

Nyengine ni Action for Justice in Society (AJISO), HUPEMEF, Community Economic Development and Social Transformation (CEDESOTA), Women Wake-Up (WOWAP), Tanzania Peace, Legal Aid and Justice Centre (PLAJC), Child Support Tanzania (CST), Elimisha.

Pia, Faidika Wote Pamoja (FAWOPA), Pemba Association for Civil Society Organization (PACSO), Tanzania Development and AIDS Association (TADEPA), TALISDA Foundation, Tanzania Rural Women and Children Development  Foundation (TARWOC) na Morogoro Paralegal (MPLC)

Katika ziara hiyo tume ilisambaza maafisa wake kwenda katika taasisi hizo ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu utendaji kazi wa taasisi hususani katika maeneo ya utoaji wa elimu kwa umma, ukusanyaji wa taarifa za matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu namna ya kutoa taarifa na ufuatiliaji.

Aidha, maafisa wa tume walitumia nafasi hiyo kuelezea kazi za tume hususani katika eneo la ushirikiano na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo kwa kuzingatia makubaliano ya mkataba.

Ziara hiyo ni ya kwanza tume kuifanya kando na ile iliyoifanya mwaka 2016 kwa lengo la kuzifanyia tathimini asasi kadhaa ili kupata zile ambazo zitakidhi vigezo vya kufanya kazi na tume, ambapo baada ya mchakato huo kukamilika tume ilipata taasisi ishirini (20) na kuingia nazo mkataba wa makubaliano mwaka 2017.