11
Sat, Jul
7 New Articles

Tume kushirikiana na sekta ya biashara

Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya akifungua mkutano huo wa wadau wa sekta ya biashara kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu njia bora ya kulinda na kuteteta haki za binadamu katika sekta ya biashara nchini uliofanyika katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es Salaam Desemba 3, 2018.

News
Typography

Tume ya haki za binadamu na Utawala bora(THBUB) imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya biashara katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa shughuli zao nchini.

Tume imetoa ahadi hiyo kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya biashara kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu njia bora ya kulinda na kuteteta haki za binadamu katika sekta ya biashara nchini uliofanyika katika ofisi zake zilizopo jijini Dar es Salaam Desemba 3, 2018.

 

Akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya  alisema  anatambua kuwa sekta ya biashara nchini inakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo ushindani mkubwa  wa kibiashara, upatikanaji wa fursa za kiuwekezaji, ufinyu wa upatikanaji mitaji na kukosekana wa masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi.

Muya aliongeza kuwa anatambua kwamba ufahamu mdogo wa sheria za nchi na namna ya utekelezaji wa sheria hizo ni changamoto ambayo imekuwa  inakwamisha kutekeleza haki za binadamu katika sekta ya biashara.

 Kwa kutambua changamoto hizo zinazoikabili sekta ya biashara, Muya aliendelea kusema kuwa, mwaka 2017 tume ilifanya utafiti kuhusu hali ya haki za binadamu na biashara nchini ili kubaini changamoto na kutafuta njia bora za kutatua changamoto hizo.

“Tumekutana hapa leo ili kuwajengea uelewa wa masuala ya haki za binadamu, kuwafahamisha matokeo ya utafiti tulioufanya kuhusu haki za binadamu na biashara nchini na kupokea maoni ili kuboresha hali ya biashara ikiwemo kulinda na kutetea haki za binadamu katika sekta ya biashara”,alisema Muya

Aidha, Muya aliipongeza sekta ya biashara kwa mchango wake katika kukuza uchumi wa kwa kushiriki kuboresha hali za maisha ya wananchi katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni nchini.

“Tume inatambua miradi mingi ya maendeleo iliyotekelezwa na sekta ya biashara kama ujenzi wa barabara, hospitali, shule na huduma za maji safi na salama kama mchango wenu kwa jami”, Muya aliongeza

“Hivyo, tume ingependa kuona mnaendelea  kuboresha maisha ya jamii kwa kuweka mikakati ya pamoja kuhusu njia bora ya kulinda na kutetea haki za binadamu katika sekta ya biashara nchini”, Muya alisisitiza

Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano huo ni  Shirika la uchimbaji wa madini nchini(STAMICO), Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Shirika la Mafuta ya Petroli nchiniTanzania (TPDC), shirikisho la viwanda (CTI), East African Cables, Hill Packaging, Export Processing Zones Authority (EPZA) na Kampuni ya Bia ya Serengeti.