11
Sat, Jul
7 New Articles

Muwakilishi IWIGIA atembelea THBUB

Kaimu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya(kushoto) akiongea na Muwakilishi kutoka taasisi ya IWGIA, Marianne Wiben Jensen katika ofisi yake Novemba 23, 2018.Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo, Alexander Hassan na aliye kati ni Afisa Uchunguzi, Florence Chaki.

News
Typography

Na Mbaraka Kambona,

Muwakilishi kutoka taasisi ya IWGIA, Marianne Wiben Jensen ameitembelea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Novemba 23, 2018.

Katika  kikao  kifupi kilichofanyika kwenye  ofisi za Tume jijini Dar es Salaam, Jensen alimueleza Kaimu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya kuwa lengo kuu la ziara yake hiyo ni kufanya tathmini ya hali ya utekelezaji wa mradi wa uchunguzi wa hadharani uliofadhiliwa na shirika hilo kuhusu migogoro ya ardhi kwa watu wanaoishi maisha ya asili nchini.

Mradi huo uliotekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 ulifanyika katika mikoa minne ambayo ni Manyara, Singida, Tanga na Kilimanjaro.

 

Wakati akieleza hali ya utekelezaji wa mradi huo, Kaimu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Hajjat Fatuma Muya alimueleza Muwakilishi huyo kutoka  IWGIA kuwa utekelezaji wa mradi huo umeshakamilika na taarifa imeshaandaliwa kinachosubiriwa ni uteuzi wa makamishna wa tume ili taarifa hiyo iweze kuzinduliwa.

Aidha katika hatua nyingine, Muwakilishi huyo wa IWGIA alitaka kujua ni maeneo gani ya utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ambayo tume ingependa kushirikiana na IWGIA.

Katika kujibu hilo, Muya alimueleza muwakilishi huyo  kuwa tume ingependa kushirikiana na IWGIA katika masuala yafuatayo; kufanya mikutano ya kampeni kuhusu haki za watu wanaoishi maisha asilia nchini ili kuihamasisha jamii kuhusu haki za watu hao, kuendelea kufanya tafiti kuhusu migogoro ya ardhi katika jamii ya Wahadzabe na Maasai.

Maeneo mengine ni  kufanya tafsiri ya tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wanaoishi maisha asilia kwa lugha ya Kiswahili liweze kueleweka kirahisi kwa jamii,kufanya  mafunzo kwa maafisa wa tume kuhusu malengo ya maendeleo endelevu yanayohusisha haki za watu wanaoishi maisha asilia na kufanya ‘Baseline Survey’ ya watu wanaoishi maisha asilia nchini.

Muwakilishi huyo alisema kuwa  maeneo hayo yote yaliyoainishwa ni muhimu na yatapewa kipaumbele.

IWGIA ni shirika la haki za binadamu linaloshughulika na uhamasasishaji, uhifadhi na ulinzi wa haki za watu wanaoishi maisha asilia duniani.