11
Sat, Jul
7 New Articles

Tume yaliahidi ushirikiano bunge la Uganda

News
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeuahidi ujumbe  kutoka Uganda uliojumuisha wabunge wanne (4) na Maafisa wawili  kutoka Serikali ya Uganda kuwa itashirikiana nao katika mchakato wa maandalizi ya muswada wa kuzuia na kupinga vitendo vya mateso na mauaji ya kutoa kafara binadamu vinavyoendelea nchini humo.

 

Tume ilitoa ahadi hiyo ya ushirikiano kwa ujumbe huo katika kikao kilichofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2018.

Akiongea katika kikao hicho, kiongozi wa msafara huo, Atiku Benard (Mb) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia jukwaa la watoto nchini Uganda alisema kuwa lengo la ziara ya ujumbe huo ni kujifunza na kubadilishana uzoefu jinsi Tume na Serikali ya Tanzania inavyopambana kuzuia matukio ya kikatili dhidi ya binadamu.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kwa sasa Serikali ya Uganda ipo katika mchakato wa kuandaa rasimu ya muswada wa kupambana na kuzuia vitendo vya mateso na mauaji ya kutoa kafara binadamu vinavyoendelea nchini humo.

Tume iliueleza ujumbe huo kuwa pindi watakapokamilisha rasimu ya muswada huo wapo tayari kuupitia na kutoa mawazo na maoni yao kwa lengo la kuboresha muswada huo.

Ujumbe huo kutoka Uganda ulikuwa na watu wafuatao: Atiku Benard (Mb), Mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayosimamia jukwaa la watoto nchini Uganda, Khainza Justine (Mb), Agori James(Mb), AcengFlorence Winnie (Mb), Tessa Kawoya, Afisa kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria ya Uganda, na Juliet Kamngisa, Afisa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria nchini Uganda.