05
Fri, Jun
5 New Articles

THBUB yatoa mafunzo kuzuia vurugu za kiitikadi

News
Typography

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kwa kushirikiana na Asasi ya Public International Law and Policy Group (PILPG) hivi karibuni imeendesha mafunzo ya uandaaji wa mikakati ya uchechemuzi (advocacy strategies) na mpango kazi wa kuzuia vurugu za kiitikadi (Violence extremism) nchini.

  Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza Februari 27, 2018 yaliwahusisha takriban washiriki 40 kutoka taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia na yaliwezeshwa na Mkufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia, Bw. Salim Othman Hamad.

Inatarajiwa kuwa iwapo washiriki watatumia vizuri ujuzi walioupata taifa litafanikiwa kujenga jamii yenye kuheshimu haki za binadamu na kudumisha amani ambayo ni tunu muhimu kwa ustawi wa nchi.

PILPG ni Asasi ya kimataifa inayojihusisha na utoaji wa misaada ya kiufundi na fedha kwa taasisi za Umma na Asasi za Kiraia zinazojihusisha na masuala ya haki za banadamu na utawala bora.