11
Sat, Jul
7 New Articles

Kaimu Balozi Atembelea THBUB

News
Typography

Mnamo Desemba 13, 2017,Kaimu Balozi ( Deputy Chief of Mission) wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Inmi K. Patterson alitembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB ) kwa lengo la kufahamu majukumu na changamoto za Tume, nafasi ya Tume katika kushauri Serikali katika kulinda, kutetea na kukuza hazi za binadamu nchini pamoja na kujua utendaji kazi wa Tume kwa ujumla.

 

Akiishukuru Tume kwa ukaribisho na mashirikiano mazuri, nakwa jinsi THBUB inavyojitahidi kutetea haki za binadamu hususani haki za kiraia na kisiasa, Mhe Patterson aliahidi kuendeleza Ushirikiano baina ya Tume na Ubalozi wa Marekani.

Kwenye mazungumzo yake na viongozi wa Tume Kaimu balozi alitaka pia kujua kitu gani Tume ingependa kupata kama msaada kutoka Ubalozi wa Marekani.

Akijibu swali hilo Mwenyekiti wa THBUB, Mh. Bahame Tom Nyanduga, alisema kwa sasa Tume ingependa kuona watumishi wake wakiwa na Uwezo na mbinu mbalimbali za Kiuchunguzi hasa kwa ngazi ya Stashahada (Masters level) pamoja na mafunzo ya muda mfupi (short courses)

Kwa upande wake Katibu wa THBUB, Bi.Mary Massey alimweleza Kaimu Barozi mahitaji na changamoto zinazokabili Tume.

Alisema, suala la ufinyu wa bajeti ni tatizo kubwa ambalo linakwamisha shughuli nyingi za Tume, ikiwemo : Kushindwa kuwafikia wananchi wengi hasa wale wa vijijini, Upungufu wa ofisi mikoani pamoja na Uhaba wa vitendea kazi.

Mhe. Patterson alitembelea Tume ikiwa ni njia ya kujitambulisha na kuzifahamu taasisi zinazohusiana na masuala ya haki za binadamu kwa kuwa ni mgeni nchini.