Premium Joomla Templates by iPage Coupon

Commission

The Commission for Human Rights and Good Governance (CHRAGG) is an independent government department, established as the national focal point institution for the promotion and protection of human rights and duties as well as good governance in Tanzania. CHRAGG was established under Article 129(1) of the Constitution of the United Republic of Tanzania of 1977 as amended by Act No. 3 of 2000.

The Commission became operational on the 1st July 2001 after the coming into force of the Commission the Human Rights and Good Governance Act No7 of 2001 as amended by Act No 16 of 2001 and Government Notice No. 311 of 8th June 2001. The Commission was officially inaugurated in March 2002 following the appointment of Commissioners by the President of the United Republic of Tanzania. download Act No. 7

KAMPENI ZA KUHAMISISHA SHUGHULI ZA KUWASILISHA MALALAMIKO KWA NJIA YA UJUME MFUPI UNAYOFANIKA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA NA VISIWANI.

17th July 2014

Tume yaendesha mafunzo ya haki za binadamu kwa watendaji wakuu wa asasi zisizo za kiserikali, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi  wa Dominic Nyakahoja jijini Mwanza. Mafunzo hayo yalifunguliwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi Mary Massay. Katika mafunzo hayo Bi. Mary Massay aliwataka washiriki waweze kuzingatia mambo ambayo yatakuwa yanayotolewa na watoa mada. Mada zilizojadiliwa katika mafunzo hayo ni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na jinsi ya kuleta malalamiko Tume kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani na Mpango Kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu. Aidha, Katibu Mtendaji aliziomba asasi hizo kuweza kushirikiana katika kupiga vita uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa kutumia njia za kuwasadia wananchi ili waweze kudai haki zao na kutoa taarifa Tume pindi haki hizo zinapovunjwa kwa kutumia ujumbe mfupi kwa njia ya simu ya kiganjani. Aidha katibu Mtendaji aliwashukuru SIDA na The Swedish program for ICT in  developing regions (SPIDER) kwa kufadhili mafunzo haya.

Tume ya Haki za Binadamu yaagana na Mtaalamu wa masuala ya ulinzi wa mtoto kutoka UNICEF.

16th July 2014

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora leo imefanya hafla fupi ya kuagana na mtaalamu wa masuala ya ulinzi na haki za watoto wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ofisi ya Tanzania Bi Rachel Harvey ambaye anahamia nchini Nigeria anakokwenda kuwa mkuu wa Kitengo cha kutetea na ulinzi wa haki za watoto.
Bi Rachel amekuwa akifanya kazi karibu na Tume katika kipindi chote cha miaka mine (4) aliyokuwa nchini, baadhi ya kazi alizofanya akiwa na Tume ni pamoja na kuratibu kazi mbalimbali kuhusiana na masuala ya haki za watoto katika mkinzano na Sheria; Mwaka 2011 Bi Rachel alishirikiana na ujumbe wa Tume kukagua magereza, vituo vya polisi, mahabusu ya watoto na shule ya maadilisho katika mikoa ya Mbeya na Iringa.
Bi. Rachel atakumbukwa sana kwa mchango wake mkubwa aliokuwa nao katika kuboresha haki za watoto nchini. Alishiriki kikamilifu katika kuandaa kanuni za sheria ya mtoto, kuwajengea uwezo wadau juu ya sheria ya mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na kushiriki katika maandalizi ya mkakati wa miaka mitano wa Haki za watoto unaoratibiwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Tume ya Haki za Binadamu itaendelea kuenzi juhudi za Rachel za kuunganisha taasisi zinazoshughulikia masuala ya haki za watoto katika mkinzano na sheria ambapo nyenzo mbalimbali za ufuatiliaji ziliandaliwa katika kufuatilia watoto katika vizuizi mbalimbali nchini.