Commission for Human Rights and Good Governance

Hello world!
Welcome to WordPress. This is your first post. Edit or delete it, then start blogging!

THBUB yaanzisha mfumo wa kompyuta kushughulikia malalamiko ya wateja
HATIMAYE Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeanzisha mfumo wa kompyuta kushughulikia malalamiko ya wateja. Mfumo huo mpya utabadili mfumo uliokuwepo awali ambao haukuwa na tija ili kuongeza ufanisi wa kufanya uchunguzi wa vitendo vya kuvunjwa kwa Haki za Binadamu.

Chini ya mfumo huo mpya ambao ulizinduliwa rasmi na Mshauri Mwandamizi wa Utawala Bora kutoka Ofisi ya Ushirikiano ya Kanada Tanzania, Bw. Maury Miloff, zaidi ya maafisa uchunguzi 100 wa Tume watapatiwa mafunzo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Amiri Manento, mfumo huo pamoja na mafunzo kwa watumishi wa Tume vitagharimu kiasi cha shilingi milioni 285 (sawa na zaidi ya dola 280,000 za Marekani).

Kwa kutumia mfumo huo, Tume itaongeza ufanisi na kutoa majibu ya malalamiko kwa kasi zaidi. “Tume imeanza kutambua umuhimu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) kwa uwezo wake wa kutoa huduma kujenga jamii yenye haki na usawa inayozingatia au kuheshimu Haki za Binadamu na kanuni za Utawala Bora,” alisema Jaji Manento.

Aliendelea kusema kuwa mabadiliko hayo ambayo ni sehemu ya mkakati wa mawasiliano wa Tume yatazingatia weledi kwa kutumia wataalamu wenye ujuzi na ufahamu hususani kwa maafisa wake wa uchunguzi na utunzaji kumbukumbu za wateja.

“Ningependa kuarifu kuwa uingizaji wa mafaili ya wateja wetu kwenye mfumo wa kompyuta lilikuwa jambo lililonuiwa na kuhimizwa kwenye mpango wa kati wa Programu ya maboresho ya Sekta ya Sheria (LSRP) iliyofadhili mradi huo kwa kiasi  kikubwa kwa kushirikiana na Serikai ya Tanzania” alisisitiza Jaji Manento.

Akifungua mafunzo hayo, Bw. Miloff ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya ufunguzi alisema kwamba mfumo wa kompyuta wa kushughulikia malalamiko unalenga kutoa taarifa kwa wadau wote kwa mpangilio unaofaa ndani ya muda unaokubalika.

Akipongeza jitihada zilizofanywa na THBUB, hususan kitengo cha TEKNOHAMA, mtaalam huyo kutoka Kanada alisema mfumo huo mpya hatimaye utawezesha kupata taarifa zilizo kwenye mafaili kwa njia ya simu na hivyo kurahisisha mawasiliano zaidi kwa kiwango cha kuwawezesha hata wateja wanaotoa malalamiko kufahamu hatua iliyofikiwa katika kushughulikia malalamiko yao ambapo muhimu zaidi ni kuwa, malalamiko yanaweza kukusanywa na Tume kutoka hata sehemu za pembezoni kabisa mwa nchi.

Suala muhimu kutambua ni ukweli kuwa Tume imepokea na kusajili idadi kubwa ya malalamiko kutoka kwa wateja wake tangu kuanzishwa mwaka 2001 ambapo zaidi ya mafaili 26,000 yenye kesi za kuvunjwa kwa haki za binadamu na kukiukwa kwa utawala bora yameshughulikiwa.

Idadi ya malalamiko kutoka kwa wateja yamekuwa yakiongezeka kila mwaka wakati uwezo wa Tume kuyashughulikia mapema na kwa ufanisi umekuwa ukipungua hivyo kuanzishwa kwa mfumo huu mpya wa kushughulikia malalamiko kwa kutumia kompyuta ni jambo lililokuja kwa wakati muafaka.